MAONESHO YA VYUO VIKUU TANZANIA (TCU)

WENGI WAJITOKEZA BANDA LA TICD KWENYE VIWANJA VYA MNAZI MMOJA.

Wakazi wengi wa Dar es Salaam wamejitokeza kwenye maonesho ambayo ya meandaliwa na Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU), na kufika  katika Banda la Chuo cha Maendeleo ya Jamii kwa ajili ya kupata usaidizi wa kujisajili ili kuweza kujiunga na chuo na kupata taarifa nyingine za muhimu.

Tunaendelea kuwajulisha na wengine kufika katika Banda letu kwa siku zilizobaki (hadi Jumamosi ya Julai 22, 2023.

Ikumbukwe kuwa hakuna kiingilio katika Maonesho haya.

Aidha, ukifika jukwaa kuu utaona Bango kubwa la TICD au waweza kutupigia simu kwa namba 0742 350 781 au 0764 642 281 na timu yetu ya TICD itakufuata na kukuongoza hadi kufika katika Banda la TICD.

Karibuni sana.

Katika picha:

Ni Prof. George Kinyashi, Naibu Mkuu wa Chuo cha Maendeleo ya Jamii Tengeru (TICD), anayeshughulikia masuala ya Taaluma ambapo leo Julai 18, 2023 amekuwa sehemu ya Timu ya maonesho kutoka Chuo cha Maendeleo ya Jamii Tengeru katika Maonesho ya 18 ya Elimu ya Juu, Sayansi na Teknolojia ambayo yanayoendelea katika viwanja vya Mnazi Mmoja, Dar es Salaam.

Prof. Kinyashi ameshiriki katika kutoa taarifa kuhusu TICD na kuwahamasisha wananchi wa Dar es Salaam kutembelea Banda la Chuo cha Maendeleo ya Jamii Tengeru kwa siku zilizobaki kwa Maonesho hayo ambazo ni Julai 19 hadi Julai 22, 2023.

Prof. Kinyashi pia ameshiriki hafla ya ufunguzi wa Maonesho hayo ambayo Mgeni Rasmi alikuwa Mhe. Prof. Adolf Mkenda (MB), ambaye ni Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia.