MAONESHO YA VYUO VIKUU TANZANIA (TCU)

WENGI WAJITOKEZA BANDA LA TICD KWENYE VIWANJA VYA MNAZI MMOJA.
Wakazi wengi wa Dar es Salaam wamejitokeza kwenye maonesho ambayo
yameandaliwa na Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU), na kufika katika Banda la
Chuo cha Maendeleo ya Jamii kwa ajili ya kupata usaidizi wa kujisajili ili kuweza
kujiunga na chuo na kupata taarifa nyingine za muhimu.
Tunaendelea kuwajulisha na wengine kufika katika Banda letu kwa siku zilizobaki (hadi
Jumamosi ya Julai 22, 2023.
Ikumbukwe kuwa hakuna kiingilio katika Maonesho haya.
Aidha, ukifika jukwaa kuu utaona Bango kubwa la TICD au waweza kutupigia simu kwa
namba 0742 350 781 au 0764 642 281 na timu yetu ya TICD itakufuata nakukuongoza
hadi kufika katika Banda la TICD.

Karibuni sana.

Katika picha:

Ni Prof. George Kinyashi, Naibu Mkuu wa Chuo cha Maendeleo ya Jamii Tengeru
(TICD), anayeshughulikia masuala ya Taaluma ambapo leo Julai 18, 2023 amekuwa
sehemu ya Timu ya maonesho kutoka Chuo cha Maendeleo ya Jamii Tengeru katika
Maonesho ya 18 ya Elimu ya Juu, Sayansi na Teknolojia ambayo yanayoendelea katika
viwanja vya Mnazi Mmoja, Dar es Salaam.

Prof. Kinyashi ameshiriki katika kutoa taarifa kuhusu TICD na kuwahamasisha
wananchi wa Dar es Salaam kutembelea Banda la Chuo cha Maendeleo ya Jamii
Tengeru kwa siku zilizobaki kwa Maonesho hayo ambazo ni Julai 19 hadi Julai 22,
2023.

Prof. Kinyashi pia ameshiriki hafla ya ufunguzi wa Maonesho hayo ambayo Mgeni
Rasmi alikuwa Mhe. Prof. Adolf Mkenda (MB), ambaye ni Waziri wa Elimu, Sayansi na
Teknolojia.

Post a Comment