JINA LA KOZI: UONGOZI WA SERIKALI ZA MITAA NA  UTAWALA BORA

Mahali: TICD Kampasi Kuu, Arusha

Muda wa Mafunzo: Juma 1

Kuanza: 02 Okt 2023, Kumaliza: 06 Okt 2023

Ada washiriki wa nje ya Nchi: 350$

Ada washiriki wa Ndani ya Nchi: TZS 700,000

Ada ni kwa ajili ya: Gharama za mafunzo, chakula na viburudisho tu.

MAELEZO YA MAFUNZO

Kwa sehemu kubwa, Viongozi wanaofanya kazi kwa tija na ufanisi ni wale wenye maarifa na ujuzi mahsusi juu ya uongozi na utawala bora. Aidha, ni viongozi ambao wanauwezo wa kuongoza watu na kusimamia rasilimali zinazopatikana katika maeneo yao ya utawala, kwa manufaa na maslahi mapana ya jamii. Tanzania inahitaji viongozi wenye weledi katika kuongoza na wenye kuzingatia misingi ya utawala bora. Kwa kutambua ukweli huu, Chuo cha maendeleo ya jamii Tengeru kimeandaa mafunzo ya uongozi,  usimamizi na utawala bora maalum kwa wawakilishi wa jamii na watendaji wengine kwenye serikali za mitaa ili kuwaongezea ujuzi na maarifa ambayo yatawasaidia kukabiliana na changamoto zinazowakabili huku wakizingatia na kuheshimu misingi ya utawala kwa maendeleo endelevu.

WALENGWA WA MAFUNZO

Walengwa wa mafunzo haya ni wawakilishi wa jamii hususani waheshimiwa Madiwani, Wenyekiti wa Halmashauri, Mameya, Viongozi na Watendaji wengine wa shughuli za kiutawala kwenye Halmashauri.

MATOKEO YA MAFUNZO

Mafunzo haya yanatarajiwa kuwawezesha washiriki:

      • Kuongeza na kuimarisha uwajibikaji wao katika kuwatumikia wananchi
      • Kupata mbinu za kufuatilia na kutathimini utekelezaji wa shughuli za maendeleo
      • Kuwa watumishi bora, waadilifu wakionyesha kwa vitendo dhana ya utawala bora
      • Kuelewa jinsi ya kuandaa bajeti, kuibua vyanzo vya mapato na kusimamia miradi
      • Kuelewa jinsi ya kutunga na kusimamia sheria ndogondogo za halmashauri zao

MADA ZITAKAZOFUNDISHA

      • Mfumo wa serikali za mitaa na uendeshaji wa shughuli zake
      • Sifa, mwenendo, kazi, wajibu, haki na stahiki za  wawakilishi wa jamii
      • Utendaji na uwajibikaji wa halmashauri
      • Mahusiano ya kiutendaji kati ya wachaguliwa na watendaji wengine wa halmashauri
      • Utungaji wa sheria ndogo ndogo
      • Elimu ya kuibua vyanzo na usimamizi wa mapato ya halmashauri
      • Sheria ya maadili, utawala bora na mapambano dhidi ya rushwa
      • Utunzaji wa kumbukumbu ili kuimarisha uongozi na utawala bora
      • Utaratibu wa ununuzi na sheria zake
      • Uandaaji wa bajeti na usimamizi wa miradi mbalimbali ya jamii.
      • Udhibiti wa msongo wa mawazo na kuinua ustawi wa afya ya akili