Na TICD, ARUSHA
Taasisi ya Maendeleo ya Jamii Tengeru (TICD) zamani ilijulikana kama Community Development Training Institute (CDTI Tengeru) ipo mkoani Arusha wilaya ya Arumeru nje kidogo ya jiji la Arusha ikiwa ni kilometa 13 kutokea mjini Arusha, kando ya barabara ya Moshi-Arusha.
Taasisi ya Maendeleo ya Jamii Tengeru ni mojawapo ya Taasisi kongwe za serikali iliyoanzishwa baada ya nchi yetu kupata uhuru kutoka kwa Mwingereza mwaka 1961.
Kwa mujibu wa masimulizi ya viongozi mbalimbali wastaafu wa Chuo cha Maendeleo ya Jamii Tengeru akiwemo Dkt. Florence Ghamunga ambaye amewahi kuwa Mkuu wa Chuo kati ya mwaka 1985 – 1986 na Bw. Salum Hamis Selenge ambaye amewahi kuwa Mkuu wa Chuo cha Maendeleo ya Jamii Tengeru kati ya mwaka 2003 – 2007, Serikali ya awamu ya kwanza chini ya uongozi wa baba wa Taifa Mwalimu J.K. Nyerere ilikuwa na mikakati ya kupambana na ujinga, maradhi na umasikini.
Kwa mujibu wa masimulizi hayo na nyaraka mbalimbali, Taasisi au kama ilivyokuwa ikijulikana zamani Chuo cha Maendeleo ya Jamii Tengeru kilianzishwa mwaka 1963 kama kituo kwa lengo la kutoa mafunzo ya muda mfupi kwa mabwana na mabibi maendeleo waliokuwa na jukumu la kuhamasisha maendeleo.
Baadhi ya miundombinu iliyopo sasa hivi ilijengwa mwaka 1964 chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa msaada wa Shirika la Misaada la Wamarekani (USAID). Lengo lilikuwa kutanua huduma ya mafunzo kwa nchi za Afrika ya mashariki, magharibi na kati.
Hata hivyo, historia inaoesha kwamba kuanzishwa kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) mwaka 1967 kulipelekea majengo haya kutotumia kwa kuwa majengo ya Kituo yalikabidhiwa kwa Jumuiya. Mwaka 1968, shughuli za Kituo zilihamishiwa chuo cha Mzumbe Morogoro na kuunganishwa na Kituo cha mafunzo ya serikali za mitaa na kuunda Kituo cha mafunzo ya Serikali za Mitaa na Maendeleo vijijini mwaka 1970.
Baada ya kuvunjika kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki mwaka 1977, majengo yalirudishwa Ofisi ya Waziri Mkuu chini ya kitengo cha Ujamaa na Maendeleo ya Ushirika (Ujamaa and Cooperative Development Division).
Kituo kilianza tena kutoa mafunzo ya Astashahada (Certificate) mwaka 1978 kikijulikana kama Chuo cha Ujamaa na Maendeleo ya Ushirika (Ujamaa and Cooperative Training Institute). Mwaka 1981, chuo kiligawanyika na mafunzo ya Maendeleo ya Jamii kwa ngazi ya Astashahada kwa miaka miwili yalianza kutolewa na Chuo cha Maendeleo ya Jamii Tengeru (Community Development Training Institute-Tengeru).
Aidha, kuanzia mwaka 1983 chuo kilianza kutoa mafunzo ya Stashahada ya juu ya Maendeleo ya Jamii (Advanced Diploma in Community Development) kwa miaka mitatu.
CDTI ilitambulika rasmi kama Taasisi ya elimu ya juu (Higher Learning Institution) mwaka 1994 baada ya mtaala wa mafunzo ya stashahada ya Juu ya Maendeleo ya Jamii kupitiwa na kupitishwa na mamlaka ya Uzimamizi wa mafunzo kwa wakati huo. Hata hivyo, Taasisi iliidhinishwa kuwa na mamlaka kamili mwaka 2013 na Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) kwa sheria namba 1 ya mwaka 2013 ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
SHUGHULI ZINAZOFANYWA NA TICD
Taasisi inafanya shughuli kuu tatu kama zifuatazo;
-
- Kuendesha mafunzo ya muda mrefu na mfupi.
-
- Kufanya tafiti na;
-
- Kutoa ushauri elekezi.
MAFUNZO YANAYOTOLEWA NA TICD
Taasisi inatoa huduma zake kwa kuzingatia taratibu na sheria zilizowekwa na mamlaka zinazosimamia elimu ya kati na juu nchini ambazo ni Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi na Mafunzo Stadi (NACTVET) na Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU). Programu za mafunzo ni pamoja na:
-
- Katika ngazi Cheti cha Awali (Basic Technician Certificate-NTA level 4) kuna program za mafunzo zipatazo saba (07 katika fani za Maendeleo ya Jamii (Community Development); Jinsia na Maendeleo ya Jamii (Gender and Community Development); Uendeshaji wa Miradi katika Maendeleo ya Jamii (Project Management for Community Development); Usimamizi wa Rasilimali Watu (Human Resource Management);Ustawi wa Jamii (Social Work); Uhasibu na Usimamizi wa Fedha (Accounting and Finance); Utawala na Usimamizi wa Serikali za Mitaa (Local Government Administration);
-
- Cheti cha Msingi (Technician Certificate-NTA level 5) mafunzo yanatolewa katika fani za Maendeleo ya Jamii (Community Development); Jinsia na Maendeleo ya Jamii (Gender and Community Development); Uendeshaji wa Miradi katika Maendeleo ya Jamii (Project Management for Community Development); Usimamizi wa Rasilimali Watu (Human Resource Management);Ustawi wa Jamii (Social Work); Uhasibu na Usimamizi wa Fedha (Accounting and Finance); Utawala na Usimamizi wa Serikali za Mitaa (Local Government Administration);
-
- Katika Stashahada (Diploma)-(NTA level 6) mafunzo yanatolewa katika fani za Maendeleo ya Jamii (Community Development); Jinsia na Maendeleo ya Jamii (Gender and Community Development); Uendeshaji wa Miradi katika Maendeleo ya Jamii (Project Management for Community Development); Usimamizi wa Rasilimali Watu (Human Resource Management);Ustawi wa Jamii (Social Work); Uhasibu na Usimamizi wa Fedha (Accounting and Finance); Utawala na Usimamizi wa Serikali za Mitaa (Local Government Administration);
-
- Kwa upande wa Shahada za Kwanza (NTA level 7 & 8); mafunzo yanatolewa katika fani za Maendeleo ya Jamii (Community Development); Jinsia na Maendeleo ya Jamii (Gender and Community Development); Uendeshaji wa Miradi katika Maendeleo ya Jamii (Project Management for Community Development);
-
- Kwa upande wa shahada za uzamili; mafunzo yanatolewa kwa katika Shahada ya Uzamili ya Maendeleo ya Jamii (Community Development); Mipango, Usimamizi na Tathmini ya Miradi (Master Degree in Project Planning, Monitoring and Evaluation); na Jinsia na Haki za Binadamu (Gender & Human Rights) ambazo hutolewa kwa kukaa darasani muda wote (Full Time); madarasa ya jioni (Evening programmes) na kwa njia ya Masafa (Blended).
SIFA ZA KUJIUNGA KWA KILA PROGRAMU YA MAFUNZO
-
- Cheti cha Awali (Basic Technician Certificate-NTA level 4)
-
- Ufaulu wa mtihani wa kidato cha nne angalau masomo manne kwa kiwango cha alama “D” au zaidi.
-
- Cheti cha Msingi (Technician Certificate-NTA level 5):
-
- Ufaulu wa mtihani wa kidato cha nne angalau masomo manne kwa kiwango cha alama “D” au zaidi
-
- Cheti cha Awali (NTA level 4) kutoka Chuo chochote kinachotambuliwa na Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) au
-
- Ufaulu wa mtihani wa kidato cha sita angalau somo moja katika kiwango cha alama E (Principal pass) na somo moja alama S (Subsidiary pass) au zaidi kwa waliomaliza kabla ya 2014 na baada ya 2015. Waliomaliza kidato cha sita 2014 na 2015 wawe na angalau alama C (Principal pass)
-
- Stashahada (Diploma)-(NTA LEVEL 6):
-
- Ufaulu wa mtihani wa kidato cha nne angalau masomo manne kwa kiwango cha alama “D” au zaidi
-
- Cheti cha Msingi (NTA level 5) kutoka Chuo chochote kinachotambuliwa na Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE)
-
- Kwa upande wa Shahada za Kwanza (Bachelor Degrees) sifa za kujiunga ni kama ifuatavyo:
-
- Waombaji wa Kidato cha Sita wawe na ufaulu wa masomo angalau mawili yenye ufaulu wa alama kuanzia D jumla ya pointi nne. Waliomaliza Kidato cha Sita mwaka 2014 na 2015 wawe na angalau ufaulu wa masomo mawili alama C pointi 4
-
- Waombaji wa Stashahada (NTA level 6) katika fani za Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia na Maendeleo, Upangaji wa Miradi, Utunzaji wa Kumbukumbu, Uchumi na Maendeleo, Ualimu, Utawala na Rasilimali watu wawe na wastani wa alama B au GPA ya 3.0 kutoka kwenye vyuo vinavyotambuliwa na NACTE au TCU.
-
- Ufaulu wa mtihani wa kidato cha nne angalau masomo manne kwa kiwango cha alama “D” au zaidi.
-
- Waombaji wa Stashahada (NTA level 6) katika fani za Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia na Maendeleo, Upangaji wa Miradi, Utunzaji wa Kumbukumbu, Ualimu, Utawala na Rasilimali watu, Uhasibu, Takwimu, Uchumi, Uchumi na Maendeleo, Utawala na Biashara na Technolojia ya Mawasiliano wawe na wastani wa alama B au GPA ya 3.0 kutoka kwenye vyuo vinavyotambuliwa na NACTE au TCU
-
- Ufaulu wa mtihani wa kidato cha nne angalau masomo manne kwa kiwango cha alama “D” au zaidi.
-
- Shahada ya Uzamili ya Maendeleo ya Jamii (Master Degree in Community Development), na Shahada ya Uzamili ya Mipango, Usimamizi na Tathmini ya Miradi (Master Degree in Project Planning, Monitoring and Evaluation), sifa za kujiunga ni pamoja na;
-
- Shahada (Degree)
-
- Stashahada ya Juu (Advanced Diploma) kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na NACTE au TCU
MIUNDOMBINU YA KUJIFUNZIA
TICD inayo mazingira rafiki na tulivu kwa kufundishia na kujifunzia inayomwezesha mwanafunzi kuwa mahiri katika nyanja ya Maendeleo ya Jamii, Upangaji na Uzimamizi wa Miradi na Jinsia na Maendeleo miundombinu kama ilivyochanganuliwa hapa chini:
-
- Kumbi za Mihadhara na Madarasa
TICD inayo madarasa na kumbi za mihadhara za kutosha zenye kutoa nafasi nzuri kwa ajili ya kujifunzia na kufundishia. Kumbi za mihadhara zilipo ndani ya Taasisi zinatumika kwa ajili ya kuendeshea mafunzo ya muda mrefu na mfupi pamoja na warsha na mihadhara mbalimbali.
-
- Maabara ya Kompyuta.
Maabara hizi zimefungwa kumpyuta za kisasa zilizounganishwa na mtandao muda wote. Hali kadhalika kompyuta za Taasisi zimewezeshwa kupakuwa vitabu na machapisho vya nakala laini kutoka kwenye mifumo ya maktaba ya Taasisi hata ikiwa hakuna mtandao (offline libray).
Matumizi ya technolojia inawezesha wanafunzi kuwa kwenye mazingira mazuri na rahisi ya kujisomea. Hata hivyo Taasisi inatoa nafasi kwa wanafunzi kujiunganishia mtandao kwa njia ya ‘’WIFI’’ ili watumiaji wengi wapate huduma ya mtandao kwa pamoja.
-
- Maktaba
Maktaba kuu ya Taasisi inayo vitabu na machapisho ya kutosha zilizopo kwenye nakala ngumu na nakala laini. Maktaba hii inayo uwezo wa kutoa huduma kwa watumiaji waliopo ndani na nje ya maktaba. Watumiaji wa maktaba wanaweza kusoma vitabu vilivyopo kwenye maktaba kwa kutumia simu janja, kompyuta mpakato au kifaa chochote kinachoweza kuunganishwa na mtandao. Matumizi ya technolojia imesaidia watumiaji wengi kutumia maktaba ya Taasisi wakati wote wa siku.
-
- Malazi
Taasisi ina uwezo wa kutoa huduma ya malazi kwa wanafunzi wanaosajiliwa kujiunga na Taasisi. Aidha, malazi kwenye hosteli za Taasisi ni kwa bei nafuu. Huduma ya malazi inatolewa kipaumbele kwa wanafunzi wageni na wanafunzi wanaosoma cheti na diploma.
Taasisi ya Maendeleo ya Jamii Tengeru ina Kituo cha Huduma Tandaa na Ubunifu wa Kidijitali kilichoanzishwa mwaka 2019 kikiwa na lengo la kuibua, kukuza na kuendeleza ubunifu, Uanagenzi na Ushirikishwaji wa Jamii ndani na nje ya Taasisi. Kituo hiki kinahudumia wanafunzi waliosajiliwa kusoma kwenye Taasisi hii lakini pia wananchi wanaozunguka maeneo ya jirani na chuo katika wilaya ya Arumeru na Mkoa wa Arusha kwa ujumla. Pia Taasisi ina Kituo cha Utafiti na Uhifadhi wa Machapisho Yahusuyo Wanawake (NWRDC). Maktaba hii ina machapisho na taarifa zinazohusu utafiti utafiti na machapisho ya wanawake zilizokusanywa kutoka sehemu mbalimbali hap nchini na nje ya nchi. Maktaba hii inasaidia pia wanafunzi kujifunza na kujisomea kupitia machapisho na vitabu.
- October 22, 2024
- By: TICD Admin
- Category:ANNOUNCEMENTS
- no comments
Post a Comment